Wednesday, March 27, 2013

JACKIE WA CHUZI ADAIWA KUIBA MUME WA MTU SIKU CHACHE TU BAADA YA KUFUNGA NDOA.

Siku tu chache baada ya Jackline Pentezel kufunga ndoa na mwanaume anayeitwa Gadner Dibibi ndoa hiyo imeanza kupata misukosuko mapema mno bila kutarajiwa. Mwanamke mmoja mkazi wa Kigogo aliyetambulika kwa jina la Mariam Omary akizungumza na mtandao wa globalpublishers alisema kuwa Jack amemchukulia mume wake ambaye ni baba mtoto wake wa miezi minne hivyo anamuomba Jack amuachie mumewe huyo ambaye ni halali yake. Mariam alisema "Hakuna asichokijua kati yangu na Dibibi, kwa usalama wake aniachie mume wangu". Nae mwanaume huyo alipoulizwa na mwandishi wa globalpublishers kuhusu sakata hilo la Mariam kudai kuibiwa mume ambaye ni yeye, Gadner alisema "Alikuwa demu wangu na kuzaa mtoto isiwe sababu, hata hivyo ukweli wa baba wa mtoto anayeujua ni mama. sikumtolea mahari wala kumvalisha pete so hana kizuizi na ndoa yangu".

 Hivi karibuni Jackline Pentezel ambaye pia ni actress alifunga ndoa ambayo wengi hawakuamini kutokana na kuwa ya ghafla sana ikiwa ni wiki chache tu baada ya kudaiwa na gazeti moja la kila wiki kuwa anajiuza hivyo baadhi ya watu kuamini kuwa amefunga ndoa hiyo ili kujisafisha na skendo hiyo. wengine pia mpaka sasa bado wanaamini ndoa hiyo ni danganya toto ingawa wenyewe na marafiki zao wa karibu wamesema ni kweli wamefunga ndoa na wanapendana sana kuliko mfano. Chanzo cha kuaminika juzi kiliiambia swahiliworldplanet kuwa ni kweli Jack amefunga ndoa. Chanzo hicho kilisema "ni kwel wamefunga ndoa".

                                                    Mariam na mwanae
Actress  Jackline Pentezel and Gadner Dibibi aliyefunga nae ndoa

No comments:

Post a Comment