Wednesday, February 6, 2013

EXCLUSIVE INTERVIEW WITH MODEL/ACTRESS NUSURA WA SIRI YA MTUNGI

Katika uigizaji tayari anajulikana kama "Nusura" jina ambalo amelipata kutokana na igizo maarufu la Siri ya mtungi linaloendelea sasa na kwa upande mwingine ni mwanamitindo maarufu nchini akijulikana kwa jina la " Ida UniQue Maeda". Hata hivyo jina lake Halisi ni Hidaya Maeda. Kisura huyu ni mshindi wa taji la Miss international Tanzania mwaka 2009 ambaye ameonekana kuwavutia watazamaji katika igizo la Siri ya Mtungi. Swahiliworldplanet ilibahatika kupata nafasi ya kuchonga na actress/model huyu anayependa kujiweka kiasili zaidi katika urembo wake. Tiririka nayo ili umjue zaidi...............SWP: Unaweza kutuambia historia yako kwa ufupi elimu yako,umri na ulianza lini uanamitindo na uigizaji?

 Ida UniQue Maeda:   Jina kamili naitwa Hidaya Maeda, nina miaka 26 mwenyeji wa Mwanza.elimu yangu ni ya o'level na nina cheti cha journalism pia diploma ya full secretary na course nyingine ndogondogo ni nyingi siwezi kuzitaja zote. Nimeanza modelling since 2006 show yangu ya kwanza ikiwa ni pilipili by Mustafa Hassannali. Kuhusu uigizaji nimeanza mwaka jana 2012 Siri ya Mtungi ikiwa project yangu ya kwanza.


SWP: Ulipataje nafasi ya kuigiza katika Siri ya Mtungi character ya Nusura?

Ida UniQue Maeda:   Nilivyopata nafasi ni kama bahati tu because director aliona picha yangu online  niliyopiga wakati najianda kwenda kwenye mashindano ya Miss international 2009 so akaipenda,ndio akaanza kunitafuta. Aliyetoa mawasiliano yangu ni designer Eskado bird by that time nilikuwa Mwanza kwa ajili ya kujifungua so hata walivyoanza kunipigia simu kwa mara ya kwanza niliona kama miyeyusho tu but simu zilivyozidi ndio nikaamini kweli wananihitaji however hawakujua kama nita-suit the character au la, na walinitaka kwa ajili ya uhusika wa Nusura pekee. so haikuwa kazi sana kufanya walivyotaka ingawa ilikuwa na ugumu kidogo.
 
SWP: Unaionaje team nzima ya igizo la Siri ya Mtungi, inatofauti na timu nyingine za watengeneza filamu na maigizo ya kitanzania?

Ida UniQue Maeda:    kwakweli timu ya Siri ya Mtungi ni ya kiwango hasa upande wa vifaa, kiukweli wanajitahidi ila siwezi kulinganisha na timu nyingine kwa sababu sijafanya kazi na kampuni yoyote zaidi ya hii MFDI so sijui hao wengine wako vipi.

  SWP: Kuna madai kuwa malipo ya wasanii wa siri ya mtungi ni mazuri kuliko ya wacheza filamu za kitanzania je unaweza kulizungumziaje hili?

Ida UniQue  Maeda:   Hilo pia siwezi kulizungumzia  kwa kuwa sijafanya kaz na hizo kampuni nyingne so sijui hao wanalipaje ila kwa hawa wa siri ya mtungi malipo yao sio mabaya.


SWP:  Baada ya siri ya mtungi una mpango wa kuwa mcheza filamu rasmi au kuwa  na kampuni yako ya kutengeneza films kama waigizaji wengi nchini?

 Ida UniQue Maeda:   Dah sijajua kwa sasa, ni mapema sana kusema hivyo since nahitaji kufikiria zaidi pia kama mume wangu akiniruhusu basi inshaallah nitaendelea, na kuhusu kuwa na kampuni  hilo pia sijajua kwa sasa Itafahamika baadae, either kuwa na kampuni ya modelling or films.


SWP: Hivi Nusura wa siri ya mtungi anashabihiana na maisha yako halisi?

Ida UniQue Maeda:   Nusura hashabihiani kabisa na maisha yangu halisi,  yupo pale kwa ajili ya kuburudisha, na kuielimisha jamii.. So hakuna ninachofanana nacho labda kwenye kuongea tu.. Ha ha ha haaaaaaaa


SWP: Ungependa kuwashauri nini waigizaji na watengeneza filamu na hata directors wa wa filamu na michezo ya kuigiza kutokana na ulichojifunza kutoka katika siri ya mtungi?

Ida UniQue Maeda:   Nimejifunza mambo mengi sana but kubwa zaidi nimependa sana namna ya kuongoza films au series. Pia nataka kufanya hivyo siku moja, kingine ni watu kuwa makini na kazi hasa tunapokuwa location watu wako makini sana na wanajua wanachokifanya, directors na waigizaji wa bongo waongeze juhudi katka ubora wa kazi zao,  pia wajaribu kuigiza mambo ambayo yanaizunguka jamii kuliko kila siku kuiga mambo ya kimagharibi zaidi.

  

 SWP: Tukigeukia katika fani yako nyingine ya uanamitindo je una mpango wowote wa kuwa mwanamitindo wa kimataifa?

Ida UniQue Maeda:   Yesss.... I wish siku moja nije kuwa international model  but sijui kwa sasa. Only God knows.....


SWP:  Unafikiri ni kwa nini models wa Tanzania bado hawathaminiwi na serikali and nini maoni yako?

Ida UniQue Maeda:  Wanamitindo wa Tanzania hawathaminiwi coz na wao wenyewe hawajitambui, Hawajui thamani yao inabidi tuamke shows za elfu 30 basi sasa!, pia bado models wengi hawajui kwanini wanafanya modelling?? Wengi wao wapo kwa ajilli ya kuuza sura tu, sasa utathaminiwa saa ngapi??..si vyema kutaka msaada wa serikali wakati sisi wenyewe hatujajua tunataka serikali itufanyie nini.....tujitambue kwanza
SWP: kuna taji lolote la urembo uliwahi kulitwaa na ni lipi na mwaka gani?
Ida UniQue Maeda:   Niliwahi kushinda taji la uniQue model 2008, pia niliwahi kuwa miss international Tanzania 2009.


SWP: kati ya Flaviana Matata na Millen Magese nani anakupa inspiration zaidi ya kuwa model wa kimataifa?

Ida UniQue Maeda:  Wote wanani-inspire but zaidi ni Flaviana Matata coz ni model ambaye anajitambua, anajithamini, mbali ya kuwa na umri mdogo lakini amethubutu, ameweza, na anazidi kusonga mbele.


                                       SWP: Ahsante sana Ida kwa ushirikiano wako kwa ajili ya mashabiki wako.
                                       Ida UniQue Maeda: Ahsante pia na karibu tena.


No comments:

Post a Comment