Wednesday, January 23, 2013

WEMA SEPETU AKIMBIWA NA MARAFIKI BAADA YA KUNUNUA GARI JIPYA

famous actress from Tanzanian film industry bibie Wema Sepetu amelianika gari lake jipya aina ya Aud Q7 lenye rangi nyeusi huku akivinjari nalo sehemu mbali mbali za jiji.Wema amekaririwa akisema anashangaa jinsi watu wanavyoumia na kutokuwa na ukaribu nae tena kisa gari hilo,Ambalo limemfanya wema atimize magari matatu ambayo ni mak x hariar.Nilikuwa na marafiki wengi walionisapoti ila gari hili lilipofika nashangaa wamenikimbia sasa hata sielewi jamani badala ya mtu kufurahi kuona mwenzio kapiga hatua ili na mimi nikubebe siku ukikwama unanichukia.Wema ambaye hakutaka kuweka wazi ni akina nani hao na wamechukizwa na nini aliishia kusema ili kujua wamechukia angalia nimewaita toka jana wakutane na manager wangu ili wapange kuna kazi nataka kuifanya nao lakini hawajaja na kuna mtu wetu wa karibu alinipigia simu kuniuliza kama nimekosana na hao watu nilipomuuliza kwanini alisema ameshangazwa kuona huyo mtu hapokei simu na badala yake anasema anazingua bila kueleza anazingua nini.
Picha za gari jipya la Wema Sepetu aina ya Audi Q7 yenye rangi nyeusi zimeonekana kwenye akaunti ya Wema ya Instagram alipokuwa beach hivi karibuni na kuiandikia caption, ‘my baby at da beach.’ Kwenye akaunti ya meneja wake Martin Kadinda pia kuna picha nyingine ya gari hiyo aliyoiandikia maneno, ‘#maisha sio manhattan…..You can creat your own Manhattan in Tz… Hata kama ni ya muda mfupi… #Kiphating.’ Gharama ya gari hilo inasadikiwa kuanzia shilingi milioni 70 na kuendelea.

No comments:

Post a Comment