Tuesday, January 22, 2013

SINTAH: BONGOMOVIE MSIPOKUWA MAKINI MTAKUFA KWA UKIMWI

MSANII asiye na bahati na wasanii wenzie hasa wa bongo movie Sintah, amesema kuwa anaiombea tasnia hiyo isikumbwe na dudu baya kama HIV na magonjwa ya zinaa, kutokana na tabia iliyopo kwasasa kwa tasnia hiyo ya kunyang'anyana mabwana na anayekosa anarudi hapo hapo na kungalia mwanaume aliyezubaa hapo bongo movie. Sintah ameyasema hayo na kudokeza kuwa hali kwa sasa ni mbaya sana maana utakuta msichana huyu anatoka na wanaume zaidi ya watatu hapo hapo katika tasnia na wakati huo huo ana waume za watu kama wawili sasa hebu jiulize mmoja akiwa nao si watakufa kama kuku alafu nikisema wanasema ninawatukana alisema sintah.
Mwanadada huyo mwenye maneno ya shombo kwenye tasnia ya maigizo japo na yeye ni msanii amefunguka ipo siku ataanza kuwataja kwa majina wasichana wachafu wa bongo movie na anadhani hiyo itakuwa ndio dawa yao. Kauli ya msanii huyo imekuja mara baada ya hivi karibuni kuzuka tabia ya dada zetu haswa waliopo katika tasnia hiyo kupiga picha za uchi na kuzitundika mtandaoni sintah alisema kuwa endapo juhudi za haraka hazitachukuliwa na wasanii hao kuacha tabia hizo basi kuna madhara makubwa yanaweza kutokea kwani baadhi ya wasanii wanafanya biashara chafu ya kutembea na wanaume wengi kwa lengo la kuendesha maisha.yao. Naomba msininukuu vibaya na wala mimi sina nia mbaya na nyie ila hali ina tisha jamani,Naomba nieleweke haya ni mawazo ambayo yanaweza kuleta mapinduzi kwa tasnia hiyo ambayo imekuwa ikipewa sifa mbaya kila kukicha na kufikia wazazi kuwakataza watoto wao kuingia katika fani
“Naipenda sana tasnia hii lakini nachukizwa na baadhi ya wasanii ambao hufanya mchezo wa kubadilisha wapenzi kama nguo, na matukio mengi machafu hufanywa na wasanii hasa pale wanapokuwa kwenye bonanza pengine mkoani au kambini,” alidai. Hata hivyo aliongeza kuwa wapo wasanii wengine ambao hufanya kazi vizuri na hawajishungulishi na ujinga wowote lakini kuna makundi mengine ambayo yapo kwa ajili ya ngono na kuwapotosha wengine. ...CREDIR:the superstarblog

No comments:

Post a Comment