Pages

Wednesday, January 16, 2013

MASTAA WA KIKE BONGO JIFUNZENI HAPA

Juzi muigizaji mashuhuri duniani kutoka bollywood TABU alikuwa katika tuzo maarufu za Golden Globe Awards 2013 akiwa katika vazi la sari ambalo ni vazi la kihindi akiwa amependeza sana mpaka kutajwa kama mmoja wa mastaa waliovaa vizuri(best dressed) na mitandao,tv na magazeti mbalimbali ya hollywood,muigizaji huyu ameshaigiza filamu kadhaa kutoka hollywood na siyo bollywood pekee. Nilichokipenda ni kuwa mara nyingi mastaa wa bollywood wanapoalikwa kwenye hafla za hollywood hujiweka kiasili ili kuutangaza utamaduni wao nje za nchi nakuwa mabalozi halisi maana Tabu alivaa vazi la mbunifu wa India na kumtangaza vizuri sana siyo huyo tu mastaa kibao wa bollywwod huwa wanavaa kikwao mara nyingi wanapokwenda hollywood mfano mzuri ni Aishwarya Rai mwenye heshima tele hollywood akiwa huko huvaa mavazi ya kihindi na hata wiki iliyopita wakati anahojiwa na kituo cha kimataifa cha Aljazeera alikuwa amevaa kikwao.ila kama angekuwa staa wa Tanzania ndio amealikwa pale kwenye tuzo za golden globe nina uhakika kuwa asingefikiria hata kidogo kuvaa vazi la kiafrika maana angeona ni ushamba achilia mbali kumfikiria mbunifu wa kitanzania amtengenezee nguo.angevaa kigauni nusu uchi na kwenda kuboronga huko uzunguni. Niseme tu kuwa hata wanamitindo wa kimataifa kutoka Tanzania kama vile Flaviana Matata, Millen Magese na wengineo wanatakiwa kufikiria sana mitindo ya kiafrika wanapopita kwenye zulia jekundu huko ughaibuni kwani bado hatuwaoni wakiwa mabalozi wazuri wa mavazi ya vitenge na khanga kama mastaa wa India. Tanzania wapo madizaina wazuri sana tuwe na uzalendo jamani."Asiyependa cha kwao ni mtumwa"
Aishwarya Rai in hollywood

1 comment:

  1. Wabongo akipata hiyo nafasi atapania atinge kimini cha nguvu ili nayeye aende na wakati kama wazungu.

    ReplyDelete