Thursday, January 24, 2013
JUSTIN BIEBER ADAIWA KUBEMENDWA NA GIRLFREND WAKE MPYA
Justin Bieber anadaiwa kuwa na girlfriend mpya ingawa bado haijawa wazi kivile hasa baada ya kudaiwa kumwagana na aliyekuwa sweetheart wake bibie Selena Gomez. Msichana anayedaiwa kutafuna penzi na justin Bieber anaitwa Milyn Jensen mwenye umri wa miaka 22 akiwa ni mwanafunzi wa chuo. Hata hivyo baadhi ya mashabiki wa justin wameanza kunong'ona na hata kuandika kwenye page yake katika mitandao ya kijamii ikiwemo twitter kuwa Milyn anambemenda Bieber mwenye umri wa miaka 18 wakiwa wamepishana kwa miaka 4, mashabiki pia wamemwambia kuwa msichana huyo ni mcharuko na hamfai hata kidogo.“Justin WTF, Milyn Jensen isnt good enough for you,” wrote one fan online.".Inadaiwa pia Milyn ndo amechangia Selena kumwagwa. Hata hivyo licha ya watu kuanza kumpa onyo kuhusu demu huyo yeye anaonekana kutojali na inadaiwa anapokutana nae humfanyia vituko vya kimahaba msichana huyo mwenye asili ya African-american.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment