Tuesday, January 22, 2013

BIG BROTHER AFRICA 2013 IS HERE...

Msimu mpya wa Big Brother Africa tayari umeanza kubisha hodi kwa wanaotaka kushiriki kuanza mchakato. shindano hilo maarufu ndani na nje ya bara la africa linatarajiwa kuanza rasmi may mwaka huu na nchi 14 zikitarajiwa kushiriki ambazo ni Tanzania iliyowahi kutoa mshindi, Uganda, Kenya, Malawi, Ethiopia,Zimbambwe, Zambia,Nigeria, Namibia, Botswana, Angola, South Africa, Sierra Leone, Ghana.baadhi ya vigezo vya kushiriki ni kama vile uwe n na umri kuanzia miaka 21,uwe raia wa nchi unayotaka kuiwakilisha, ujue kuzungumza kiingereza vizuri, uwe na passport ya kusafiria au uwezekano wa kuipata kabla ya mwezi march kuisha, uwe mcheshi, mvumilivu na shabiki wa shindano hilo. form za kujiunga zinapatikana www.africamagic.tv/bigbrother .pia fomu za kujiunga zitapatikana katika office za MultiChoice katika nchi zinazoshiriki kuanzia february mosi mwaka huu. Huu ni msimu wa 8 wa shindano hilo tangu kuanzishwa kwake. Do you want to be a superstar? this is your lifetime chance....

No comments:

Post a Comment