Wednesday, January 23, 2013

AKI NA UKWA WALA SHAVU VODACOM

waigizaji wa filamu hasa za comedy swahiliwood Nicholous Ngoda maarufu kama Ukwa wa Tanzania na mwenzake Meya Shabani maarufu kama Aki wa Tanzania wamepata mchongo wa kufanya kazi na kampuni ya Vodacom Tanzania. actors hao machachari wawapo mzigoni wamealikwa kutumbuiza katika tamasha la kukusanya pesa kwa ajili ya shule zisizo na maabara ambalo litaratibiwa na kampuni ya vodacom na litaanzia jijini Dar es salaam na baadaye litatia team mikoani ingawa tarehe rasmi bado haijawekwa wazi na lini.Hawa ni wasanii pekee walioalikwa kwa upande wa filamu, pia kutakuwa na burudani nyingine kedekede kutoka kwa wasanii wa ngoma za asili na sarakasi.Wasanii hawa watalipwa kwa kila show watakayoifanya ingawa bado haijajulikana wamekula deal la uzito kiasi gani. Nicholous(Ukwa) akichonga live na swahiliworldplanet alisema"ni kweli tumealikwa kufanya burudani ya vichekesho na Muziki katika tamasha litakalo ratibiwa na VODACOM. Nia nikukusanya fedha zitakazo pelekwa kwenye shule ambazo zinakabiliwa na tatizo la maabara. Tamasha hilo litaanzia hapa Dar es salaam kisha tutatembelea na mikoani. Hivyo tunawaomba wananchi wajitokeze pale watakapotangaziwa mahali tamasha litakapofanyika, pia kutakuwa na Burudani nyingine kama ngoma za asili na sarakasi."

No comments:

Post a Comment