Saturday, December 22, 2012
WAIGIZAJI WA TANZANIA NA KUTOKUJUA KIINGEREZA
Mara nyingi nimesikia sana baadhi ya watu,waigizaji wenyewe na hata baadhi ya vyombo vya habari yakiwemo magazeti hasa ya udaku na watangazaji wa radio na TV wakizungumzia au kuponda na kulaumu kuwa waigizaji wa Tanzania hawajui kiingereza hivyo hawataweza kuigiza filamu na wenzao wa nchi nyingine kama vile NIgeria au hollywood na hata bollywood.Ningependa kueleza kuwa filamu siyo kujua kiingereza au lugha yoyote ile bali filamu ni kipaji kinachoshawishiwa na elimu na kujiamini kwa mtu binafsi pamoja na ubunifu. Tanzania ina waigizaji wengi sana wenye vipaji sema tatizo ni woga,kutojiamini pamoja na upotoshaji kutoka kwa baadhi ya waaandishi wa habari na watangazaji wa filamu wanaoona ili muigizaji awe wa kimataifa ni lazima ajue kiingereza, na tatizo hili linasababishwa kwa kiasi kikubwa na waandishi wengi au watangazaji kutosomea uandishi wa habari kuhusu filamu au kutopenda kujisomea. kutokujua lugha fulani katika utengenezaji wa filamu hakuwezi kumuathiri muigizaji au inaweza kutokea lakini kwa asilimia chache sana ambazo hazina uzito maana muigizaji huangalia script na dioloji na kukariri huku akipewa maelekezo ya vitendo na muongozaji wa filamu nini afanye, hivyo basi lugha inaweza kuwa tatizo kwa muongozaji/director na siyo muigizaji maana director ndiye anatakiwa kuelewa kila kitu ili kutoa maelekezo kwa waigizaji, na ndiyo maana hata waigizaji wengi wa hollywood au india wakihojiwa kama wana mpango wa kuwa waongozaji wa filamu wanasema hawana na majibu yao ni kuwa uongozaji wa filamu ni kazi ngumu kuliko uigizaji na inahitaji weledi mkubwa tofauti na hapa kwetu kila mtu anataka kuwa muongozaji. Mfano muigizaji wa kike kutoka bollywood SRIDEV(49) ambaye ndiye anasemekana kuwa superstar wa kwanza mwanamke bollywood na kutamba sana kuanzia miaka ya themanini na mwanzoni mwa miaka ya tisini amecheza filamu nyingi sana ambazo siyo za lugha ya kihindi na filamu hizo kupata appriciation kutoka kwa film ctitics ndani na nje ya India.
Pia kitalaamu kuna watu wanaitwa voice actors and actresses ambao kazi zao ni kutumika kwa sauti zao badala ya waigizaji kutokana na sababu maalum kama vile lafudhi flan ambayo muigizaji anayo lakini haitakiwi kutumika lakini muigizaji husika ndiyo anatakiwa aigize au matakwa ya director tu ili kuleta vionjo vipya kwa watazamaji. mfano kuna baadhi ya waigizaji wa Tanzania wanashindwa kucheza na sauti zao katika filamu kwa hiyo wanaweza kuwekewa sauti za watu wengine/dubbed voice. kwa mfano tatizo la sauti linaonekana kwa baadhi ya waigizaji kama vile Ray kushindwa kucheza na sauti kutokana na uhusika au mazingira flani katika filamu alizoigiza licha ya kuwa muigizaji mzuri, Wema Sepetu kuna baadhi ya characters/filamu sauti yake haitakiwi isikike ila ya mtu mwingine bali yeye anatakiwa aigize vitendo pekee, kwa ujumla waigizaji wapo wengi na kuwekewa sauti ya muigizaji mwingine si lazima uwe na tatizo bali ni ubunifu wa muongozaji wakati mwingine ili kuleta ladha mpya.---
SRIDEV
SOME OF TANZANIAN FILM STARS
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment