Pages

Wednesday, December 10, 2014

JB Jacob Stephen Afunguka Baada Ya Ujumbe Wa Zamaradi Mketema.

Baaada ya Zamaradi Mketema kutoa maoni yake HAPA kuwa waigizaji wakubwa nchini kwanini hawaendi kimataifa licha ya kukubalika nchini akiwemo JB, Sasa JB pia amefunguka hayo hapo chini...........


"Kwanza napenda niwashukuru wote kwa jinsi mnavyotuwazia mema.kwanza naomba nichukue nafasi hii kuwapongeza waigizaji wote wa Tz.na waandaaji wa filam kwa kuthubutu kutengeneza filam hizi ktk mazingira magumu.Najua watanzania wengi wangependa kuona tukipeperusha bendera nje,lakini naomba muwape wasanii muda.Tasnia hii ni changa na ina changamoto ambazo. 

Zinakatisha tamaa.hebu tujiulize kwa nn wasomi wengi waliosomea filam udsm na bagamoyo hawafanyi filam hizi.wasambazaji wengi wakubwa mamu,wananchi na hata hans pop walijaribu wakakimbia.kuna producer mkubwa hapa nchini john riber ambaye ametengeneza filam kama neria na yellow card lakin naye ukimwambia njoo kwenye hizi filam atakupa jibu.

Nakubali tuna makosa mengi kama ubora wa filam zetu na stori.lakini nataka niwaambie mazingira ya kufanya filam bongo yanakatisha tamaa.wizi wa kazi zetu umezidi na wasambazaji wengi wamekimbia.Binafsi najipanga kuwa mtayarishaji zaidi kuliko mwigizaji kwa sasa kupitia jerusalem films .na ndio maana filam nyingi natoa nafasi kwa vijana ambao kama mabadiliko ya sera yafilam yatafanywa watatuwakilisha nje.kiswahili kisichukuliwe poa kwani kina nafasi kibwa sana.

Tukumbuke sharuk khan ni actor tajiri2 dunian lakini filam zake niza kihindi.hebu sote tusaidiane kupambana na changamoto hizi na tuanze na E.Africa kwanza huku tukiboresha.Wasomi wa filam msikimbie njooni tuanze wote.na tuwape moyo wasanii wetu waliojaribu kusimamisha tasnia hii kwa vimtaji toka mifukoni mwao na vipaji walivyopewa na mungu bila msaada kutoka popote..Asanteni kwa kutuunga mkono kwemye filam zetu."

No comments:

Post a Comment