Wednesday, October 8, 2014

Timoth Conrad Aelezea Faida Za Kujiunga Na TCA Na Tofauti Yake Na Bongo Movie Unity.

Tico ankiwa na Dokii
"Heri kujiunga na TCA kuliko kung’ngana kubaki bongo movie unit.

Wakati huu si wakati wa kujiunga na umoja ambao hauna faida yoyote kama ilivyo kwa bongo movie unit, maslahi ya watu wa chache ndio yaliyopelekea kuundwa kwa bongo movie unit hivyo watu wasitarajie kupata maslahi yoyote eti kisa wamejiunga.

Timamu casting agency  inatambulika na inautambua umuhimu wa TAFF (Shirikisho la filamu Tanzania) tofauti na Bongo movie ambayo imekuwa ikipingana na shirikisho bila kujua umuhimu wake. TCA imeanzishwa mahususi kwa kuonyesha utofauti, kwani msanii anapojiunga na TCA anapata faida nyingi kama ifuatavyo.

TCA itahakikisha msanii wake anapata elimu ya sanaa yake kwa ujumla, pamoja na kuendeleza kipaji chake kitaaluma katika namna mbali mbali.

TCA itamtafutia Msanii  kazi za kisanii nchini pamoja na nje ya nchi kwenye mashirika, makampuni, waandaji binafsi wa filamu na matangazo ya aina mbali mbali.

TCA Itahakikisha inamtangaza msanii katika njia mbali mbali ili kumfanya atambulike na jamii na kuhakikisha anajulikana yeye pamoja na kazi anazozifanya.

TCA kupitia mwanasheria wake ambaye anawasimamia wasanii wote, Itahakikisha msanii anapata haki zake za msingi hasa anapokubaliana na mteja wake ambaye atataka kumshirikisha katika kazi yake.

Wasanii wote wa TCA wanavitambulisho vinavyowatambulisha popote kwani mpaka sasa TCA imeshatanua wigo wake kwani inamiliki wasanii kutoka nchi tatu tofauti ambazo ni KENYA, TANZANIA, SOUTH AFRICA. Na bado mipango inaendelea ya kuhakikisha inawasanii kote duniani.

Tangu kuanzishwa kwa TCA mpaka sasa imeshaanza kutimiza ndoto za baadhi ya wasanii waliojiunga.

MFANO.
Hivi karibuni wasanii kumi na tano kutoka walichaguliwa kushiriki katika TANGAZO la TUSKER (Fanya kweli).

Wasanii watano kutoka TCA walipata nafasi ya kushiriki katika filamu ya MBWA MWITU iliyoandaliwa na Kajala Entertainment.

Wasanii saba kutoka TCA walipata nafasi ya kushiriki katika wimbo wa dokii ambao anatarajia kuupeleka katika masoko ya kimataifa kutokana na uhalisia wake wa kuonyesha uafrica ipasavyo. (wasanii hao hawakutaraji hata siku moja kukutana na dokii lakini TCA imewakutanisha nae)

Wasanii kumi wa TCA wamepata nafasi ya kushiriki katika wimbo wa kundi la wanamuziki linalokuja kwa kasi la X MEMBERZ. Ambapo wasanii wa kundi hilo pia wamejiunga na TCA.

Wasanii zaidi ya sita wa TCA wameshaonekana kwenye gazeti katika kuwatangaza kitu ambacho hakikuwahi kutokea katika maisha yao.

Wasanii 3 wa TCA wamepata nafasi ya kuchaguliwa kushiriki katika filamu itakayoandaliwa nchini Kenya  hivi karibuni.

Upo umuhimu mkubwa wa kujiunga na TCA hasa kama msanii anataka maendeleo yake na kufikia level ya kimataifa kama walivyo wasanii wengine wakubwa duniani ambao walipata nafasi ya kuonyesha vipaji vyao kupitia agency mbalimbali ambazo zimekuwa zikiwahangaikia katika kuwatafutia kazi na kuwapatia elimu ili waweze kufanya kazi zao za kisanii vizuri na hatimaye kuwa na mafanikio makubwa.

Mpaka sasa TCA imeshapata wadhamini ambao wanashirkiana nao katika matangazo na kuwafanya wasanii waliojiunga kutambulika."

Angalia picha za wasanii hao walio chini ya Timamu Casting Agency chini ya Timoth Conrad

Hongereni Timamu African Media na Timamu Casting Agency kwa hatua hii ............

No comments:

Post a Comment