Pages

Wednesday, October 1, 2014

Rose Ndauka Afunguka Baada Ya Kumwagana Na Malick Bandawe.

Rose Ndauka
Mapema wiki hii habari zilikuwa ni kumwagana kwa actress maarufu nchini Rose Ndauka na mpenzi wake wa siku nyingi Malick Bandawe ambaye pia walivalishana pete ya uchumba na kujaaliwa mtoto mmoja wa kike anayeitwa Naveen.
Katika kutengana huko Malick ambaye pia ni msanii wa Bongoleva akijulikana kwa jina la Chiwa Man ndiye aliyezungumza kuhusu kutengana kwao kuwa aliamua kubwaga manyanga baada ya kukalishana na mwenzake kuhusu mustakabali wa penzi lao lakini hakuona mwanga mbele yao. Sasa Rose Ndauka mmoja wa waigizaji wenye vipaji vya kuigiza nchini amezungumza na Bongo5 kwa kusema.........

"Ni kweli tumeachana hivi karibuni, kuna sababu ambazo zimetufanya mahusiano yetu yaishie hapo, tumekaa chini na kuzungumza lakini hicho ndicho tumeona ni kitu cha kufanya na cha busara"

                                                         Rose na Malick Bandawe
Like our Facebook page Swahili World Planet for more updates about Tanzanian movie stars' latest gossips, news, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.

No comments:

Post a Comment