Monday, October 6, 2014

Davina: Naichukia Sana Club Ya Bongo Movie Unity Ni Maslahi Ya Watu Wachache.

Davina
Club ya Bongo Movie Unity yapumulia mashine !....well wasanii wameamua kujitoa muhanga kueleza ukweli kila mtu akiamua liwalo na liwe lakini aseme ukweli juu ya Club hiyo ambayo kwa muda mrefu inadaiwa kutotoa ushirikiano wa kutosha katika Shirikisho la Filamu Tanzania
linalopigani maslahi ya wasanii wote na tasnia ya filamu nchini. Juzi Davina Halima Yahaya alitoa dukuduku lake baada ya na leo karudia tena kwa kuandika ......

"Jamain eti mimi hapa naambiwa eti nimeitukana Club ya Bongo Movie Unity hivi kuongea ukweli ndo matusi... niliongea ukweli hali ilivyo na ninarudia tena sina faida na Bongo movie unity..kumejaa ubinafsi na chuki hilo lipo wazi tunajuana misibani na ushuhuda ninao..naichukia Bongo movie unity, siyo club ambayo tuliitegemea iwe..mnanufaika wachache na roho zenu mbaya..narudia tena #ushahidi ninao wa mambo yote...#mnajijua"

Kundi la Bongo movie Unity ni sehemu ya kikundi kidogo tu katika tasnia ya filamu nchini wasanii wa kundi la Bongo movie unity wengi ni wale wenye majina huku wasanii wengi wakiwemo wale wachanga kuweka nguvu na matumaini yao katika Shirikisho la Filamu Tanzania(TAFF) ambalo ndio kubwa na chombo mama cha tasnia ya filamu nchini, mikakati yake ni kupigania maslahi ya wasanii wote na tasnia ya filamu nchini kwa ujumla, TAFF inaundwa na vyama mbalimbali vya wasanii wa filamu nchini lakini kundi la Bongo movie unity inadaiwa sio mwanachama sababu zikidaiwa ni kujiona ni maarufu na kila kitu huku wakiishia. Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania ni Simon Mwakifwamba huku aliyekuwa mwenyekiti wa kundi au club ya Bongo Movie Unity Steve Nyerere akijiuzulu hivi karibuni kwa madai ya kula pesa za kundi hilo kinyume na taratibu

No comments:

Post a Comment