Sunday, October 26, 2014

Msanii Ally Dex Lulenda Aja Na Filamu Yake Ya Mwisho "Chaguo Langu".

Msanii wa filamu za kiswahili nchini Denamrk Ally wa kampuni ya T.A.O Films anakuaja na filamu yake mpya iitwayo Chaguo Langu. Hata hivyo amesema ni filamu yake ya mwisho kufanya kutokana na mambo mengine kumbana ataachana kwanza na mambo ya filamu. Akizngumza na Swahiliworldplanet, msanii huyo alisema......


"Nimeamua kuja na filamu yangu mpya hii ndio filama yangu ya mwanzo na mwisho,nimeamua ku-stop na mambo ya filamu kwasababu nina kazi nyingine ninazofanya kwasasa, sikwamba nimechoka na mambo ya filamu bali nimeamua iwe hivyo.
kuazia mwaka 2011 hadi sasa nimefikia kutengeneza filamu 12, nimekuza vipaji vya wasanii wangi tu hapa Denmark.

Na filamu hii ni filamu ambayo inahusu mila na ndisturi za kiafrika.
ni stori inayohusu kijana wa kicongo kuoa msichana wa kinyarwanda, lakini familia ya mvulana haikupenda kijana wao aoe msichana wa kinyarwanda. lakini mvulana aliamua kumuoa msichana huyo bila kujali familia yake na kabila ya msichana. Mvulana alitengwa kwao na baada ya miezi mitatu msichana akajifugua mtoto wa kiume, lakini msichana akafariki na mtoto akabaki duniani. Mvulana akaamua kwenda na mtoto wake nyumbani wazazi wake walipo, swali kwa wazazi wake ikawa ni je mtoto huuyo ataitwa mcongomani au mnyarwanda. Jina la filamu ni "Chaguo Langu"



No comments:

Post a Comment