Pages

Friday, October 10, 2014

Modest Bafite Adaiwa Kuwa Mwakilishi Mzuri Wa Congo Katika Filamu.

Modest
Baadhi ya mashabiki wa filamu nchini Congo wanadaiwa kumtambua Modest Bafite kuwa ndie mwakilishi.wa nchi yao katika suala zima la sanaa ya filamu. Kwa mujibu wa chanzo kimoja walisikika wakongomani wakipiga hizo story baada ya kumaliza kutazama filamu aliyoshirikishwa Modest nakukubali kipaji chake. Walipoulizwa .kwanini wana msema modest peke yake wakati watanzania wanawatambua wakongomani wawili akiwemo Patcho Mwamba na Modest, mmoja wao alisema


"Unajua Modest amekuwa maarufu nakuonekana kuwa yeye ndie mwakilishi wa nchi.yetu kwasababu ametoka sehemu inayozungumza Kiswahili, na hiyo ndio sehemu kubwa yenye wadau wengi wa filamu za Tanzania na pia ndio sehemu iliyojikita na mambo ya sanaa"

Aliongeza kwa kusema "Patcho tunamjua pia lakini yeye ametoka sehemu isiyojua vizuri Kiswahili halafu tena wao wanajihusisha sana na.masuala ya muziki, Isitoshe pia Modest Sanaa ameianzia nyumbani kwahiyo umaarufu wake ulianzia.nyumbani tofauti na Patcho alieanzia tz"

Alipotafutwa Modest nakuulizwa kuhusiana na issu hiyo yeye alisema
"Mimi ninachokifahamu ni kwamba mimi na Patcho tunaiwakilisha nchi yetu, Hata kama ni kweli hatujatoka mkoa mmoja lakini sote ni Wakongomani na sisi ni ndugu, natunashirikiana kama watu wa nchi moja,pia Kuna filamu tutacheza pamoja hivi karibuni ili kuonesha wakongomani kuwa sisi ni kitu kimoja natunaiwakilisha Nchi yetu"


No comments:

Post a Comment