Tuesday, October 7, 2014

Mama Wema:Diamond Kumuoa Wema ni Mil.100: Nipo Tayari Kuolewa Bure: Wema Sepetu.

Mama Wema na Wema Sepetu
Latest buzz is that Diamond Platnumz kumuoa Wema Sepetu ni lazima atoe shilingi milioni mil. 100. Kwa mujibu wa gazeti moja ni kuwa mama Wema sepetu anataka mahari ya milioni 90 na ushee ili binti yake huyo asiyechuja umaarufu awe mkwe wa mama Diamond.
Inadaiwa kuwa sherehe za birthday za Wema na Diamond zilizofanyika hivi karibuni na kugharimu pesa nyingi ndiyo zinadaiwa kumtia tamaa mama Wema na kutaka mahari hiyo kubwa kwa madai kuwa Diamond anazo pesa hashindwi kutoa pesa hiyo ili kumuoa Wema ambaye umaarufu wao wote wawili ni mkubwa sana hapa Tanzaia huku umaarufu wa Diamond nje ya Tanzania ukiwa mkubwa sana kuliko wa Wema.

Hata hivyo habari zaidi zinadai kuwa Wema mwenyewe yupo tayari kuolewa hata bure na Diamond huku mama mtu akitaka pesa hizo kubwa zinazotosha kujenga nyumba ya maana.


Like our Facebook page Swahili World Planet for more updates about Tanzanian movie stars' latest gossips, news, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.

No comments:

Post a Comment