Pages

Wednesday, October 22, 2014

Kimenuka! Diamond na Nay Wa Mitego Watakiwa Kurudisha Sare Za Jeshi, Babu Tale Asekwa Ndani !

Kimenuka! Baada ya Diamond Platnumz na Nay Wa Mitego kuvaa sare za jeshi juzi katika tamasha la Fiesta inadaiwa jeshi limewataka kurudisha sare hizo na pia Babu Tale meneja wa Diamond anadaiwa kushiliwa polisi kwa suala hilo ingawa taarifa zinadai kuwa wasanii hao waliomba kibli kabla ya kuvaa na hivyo hata wao wanashangaa nini kimetokea tena.

Akizungumza na Bongo5 Nay Wa Mitego amesema "limekuwa tatizo kubwa sana, kuna watu tu wajinga wanachochea hivi vitu, ilimradi tu wote wawili mimi na Diamond tumeshapewa warning, tunatakiwa kurudisha zile nguo na kupeleka tu vitu vya watu, tutazipeleka"

"Babu Tale alikamatwa tangu jana, yupo polisi, tutajua cha kufanya kwasababu nimeona Diamond nae alikuwa ananipigia kwahiyo sijajua watu wamempa ushauri gani lakini hili suala linaisha tu, unajua hatujafanyia uhalifu, tulikuwa kazini sawa may be inawezekana tuna makosa alkini sio zile nguo zote zilikuwa ni za jeshi, kwa hiyo tutajua tu cha kufanya tutapata jawabu" aliongeza Nay Wa Mitego

Kuhusu habari kuwa walikuwa na kibali awali kabla ya kupanda jukwaani Nay alisema "Ndiyo maana nakwambia kuna vitu vipo katikati hapa sisi wenyewe hatuelewi nini kinaendelea"


Like our Facebook page Swahili World Planet for more updates about Tanzanian movie stars' latest gossips, news, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.

No comments:

Post a Comment