Pages

Monday, October 13, 2014

Diamond Atafuta Nyumba Ya Kifahari Kumpangia Meninah, Wema Sepetu Azuzuliwa Na Gari La Birthday.

Habari mpya zinasema kuwa bado moyo wa Diamond Platnumz umemzimikia msanii wa muziki wa kizazi kipya mwenye figa matata Meninah licha ya wawili hao kukanusha mara kadhaa.

Inadaiwa kuwa Diamond kupitia watu wake wa karibu na wasiri wake anafanya juu chini kumpan
gishia Meninah nyumba ya kifahari aidha maeneo ya Mikocheni au Mbezi beach jijini Dar es salaam ili Meninah ajue ni kaisi gani moyo wake hauna hali juu yake na pia kumnunulia gari la kutembelea ili asijisikie vibaya baada ya kumnunulia Wema !

Habari zaidi zinadai kuwa Diamond ambaye umaarufu wake mwaka huu umevuka mipaka ya nchini nyingi bado anaona Meninah anafaa kuwa mke wake kuliko Wema Sepetu, Na kwa mujibu wa vyanzo inadaiwa hata gari alilompa Wema Sepetu kama zawadi hivi karibuni kwenye birthday yake ilikuwa ni kutaka media na wafuatilia mambo ya watu hususani mastaa wanyamaze wakidhani Diamond hapindui wala hapumui kwa Wema Sepetu ila Meninah ndiye anadaiwa kumuweza Diamond ndani ya moyo wake.


Like our Facebook page Swahili World Planet for more updates about Tanzanian movie stars' latest gossips, news, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.

No comments:

Post a Comment