Pages

Sunday, September 28, 2014

Odama Aendelea Kumlilia Rachel Haule, Amwaga Chozi Kaburini Kwake.

Odama
Juzi Ijumaa star wa filamu nchini Odama Jennifer Kyaka pamoja na familia ya marehemu Rachel Haule aliyekuwa muigizaji wa filamu waliandaa misa ya kumuombea Rachel katika kanisa la Anglikana lililopo Magomeni Mwembechai, Dar es salaam na baada ya hapo kuelekea makaburi ya Kinondoni kuweka msalaba juu ya kaburi la Rachel.
Hata hivyo Odama alishindwa kujizuia na kuishia kuangua kilio makaburini hapo kutokana na ukweli kwamba yeye na Rachel walikuwa marafiki wakubwa sana na katika mazishi yake alijitoa sana na hivi karibuni pia alijitolea kulijengea kaburi la Rachel.

Wasanii wengine wa filamu waliokuwepo eneo hilo ni pamoja na Johari, Kupa, Mike Sangu, Badra, muongozaji wa filamu Lamata, Steve Nyerere, Neema Wa 20% na wengineo.

No comments:

Post a Comment