Pages

Tuesday, September 30, 2014

Nisha Awaacha Watu Midomo Wazi !

Nisha
Muigizaji wa filamu nchini Nisha Salma Jabu juzi aliwaacha watu hoi wakati wa utoaji wa tuzo za Action And Cut Viewers Choice Awards zilizofanyika Sunrise Kigamboni.
Baada ya kutajwa jina lake kuwa ndiye mshindi wa mchekeshaji bora wa kike(Best comedienne) Nisha alionekana kupagawa kwa furaha ya kutoamini huku baadhi ya watu wakimshangaa starhuyo kwa furaha aliyokuwa nayo. Hata hivyo Nisha aliweka wazi kuwa hakuamini kama kuna siku atakuja kupata tuzo kutokana na kazi zake za filamu ambapo amesema anajitahidi kufanya akazi bora kila siku.

Nisha na Haji Adam(Baba Haji) ambaye alipata tuzo ya best supporting actor

No comments:

Post a Comment