Friday, September 5, 2014

Dokii Amzawadia Kiwanja Lucy Komba Katika Kitchen Party Yake.

Muigizaji maarufu wa filamu nchini Dokii amemzawadia kiwanja star mwenzake wa filamu nchini Lucy Komba katika Kitchen yake iliyofanyika juzi katika ukumbi wa makumbusho ya taifa. Kitchen party ya Lucy Komba ilifunika kwa kutawaliwa na utamaduni wa kitanzania.
Dokii ni rafiki mkubwa wa Lucy Komba na mwenyewe amesema wametoka mbali hivyo aliamua kumzawadia kiwanja kilichopo Bagamoyo kama kumbukumbu ya urafiki wao.

Akizungumza na Globalpublishers Dokii aliyetoa performances nzuri katika filamu za Mdundiko na Kisate alisema "Mimi na Lucy tumetoka mbali, tumeshirikiana katika mengi na kudhihirisha upendo wangu kwake namzawadia kiwanja cha eka moja kilichopo Bagamoyo, naamini itakuwa ni kumbukumbu nzuri ya urafiki wetu"


Harusi ya Lucy Komba na mchumba wake mzungu raia wa Denmark inatarajiwa kufanyika kesho Jumamosi, Jijini Dar es salaam na sherehe nyingine kufanyika Denmark.

Lucy Komba katika Kitchen Party yake
Like our Facebook page Swahili World Planet for more updates about Tanzanian movie stars' latest gossips, news, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.

No comments:

Post a Comment