Pages

Tuesday, July 1, 2014

RJ Kwafukuta Moshi ! Chuchu Aingilia Majukumu Ya Kampuni, Johari Amtaka Ray Wagawane Mali.

Ray na Chuchu
RJ Film Company kwafukuta !...Habari mpya zilizoanza kuenea mitandaoni ni kuwa RJ Company inayomilikiwa na Vicent Kigosi "Ray" na Blandina Chagula "Johari" kunafukuta moshi mzito sababu ikiwa ni penzi la Ray na Chuchu Hans.

 Inadaiwa kuwa kwasasa Johari anataka kugawana mali za kampuni hiyo na Ray ili kuchukuwa hamsini zake baada ya kuchoshwa na mbwembwe na tambo za Chuchu katika kampuni hiyo licha ya mwanzoni kukubali matokeo kuwa ni wapenzi yeye abaki tu kama mmoja wa wamiliki wa kampuni. Inadaiwa kuwa Chuchu amejivika cheo cha ukurugenzi wa kampuni hiyo kiasi cha kuwaamrisha wafanyakazi wa kampuni hiyo nini cha kufanya pasipo ruhusa ya Ray na Johari ambao ndiyo wakurugenzi halisi na moja ya watu waliosaidia kwa kiasi kikubwa kuleta mapinduzi ya filamu za kitanzania kupitia kampuni hiyo.

Inadaiwa kuwa kadiri siku zinavyozidi kwenda ndivyo Chuchu anavyozidi kumuonyeshea dharau Johari kitu ambacho inadaiwa sio sahihi kwasababu mwanzoni Johari alidhiria Chuchu kufanya filamu za kampuni hiyo bila kinyongo kiasi cha Chuchu kujipatia jina kupitia filamu alizocheza na Ray.

Hata hivyo Swahiliworldplanet imeshindwa kuwapata wahusika ili kutolea ufafanuzi madai hayo.

                                                                           Johari
Like our Facebook page Swahili World Planet for more updates about Tanzanian movie stars' latest gossips, news, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news

No comments:

Post a Comment