Pages

Tuesday, July 1, 2014

Odama Hataki Kumuanika Hovyo Mtoto Wake Mitandaoni

Habari mpya ni kuwa muigizaji maarufu nchini Odama Jennifer Kyaka hapendi kumuanika hovyo mtoto wake mitandaoni kama baadhi ya mastaa wenzake. Haijajulikana sababu ingawa hata Odama mwenyewe waandishi wengi wamekwama kuandika habari za maisha yake binafsi tofauti na baadhi ya wasanii wenzake ambao kila kitu hukizungumza kwenye media.

Kwa upande mwingine filamu mpya ya star huyo inayoitwa Inside itatoka tarehe 10 mwezi huu wa July. Odama ameandaa filamu hiyo kupitia kampuni yake ya J-Film 4 Life huku akishirikiana na Davina Halima Yahaya, Dullah wa Planet Bongo, Ben Branco, Masinde, King Majuto na marehemu Rachel Haule katika movie hiyo. usikose kununua nakala yako halisi

Like our Facebook page Swahili World Planet for more updates about Tanzanian movie stars' latest gossips, news, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news

No comments:

Post a Comment