Thursday, July 24, 2014

Naitumia Fursa Kuwekeza Katika Ardhi Na Ujenzi Na Sio Kushindana Kuvaa Na Kwenda Club: Nisha

Nisha
Star mkubwa wa filamu Tanzania Salma Jabu Nisha amesema kuwa anaitumia vizuri fursa anayoipata sasa katika kazi zake za filamu kwa kuwekeza kwa ajili ya maisha yake ya baadae hususani katika ardhi na ujenzi na sio kushindana kuvaa, kwenda club na starehe nyinginezo zisizo na maana kama baadhi ya wasanii wengine halafu baadaye wanaishia kulalamikia maisha wakati wao wanaigiza maisha kwa kuendekeza starehe.

Akizungumza na Swahiliworldplanet Nisha amesema kuwa katika sanaa ya filamu hawezi kuwa juu siku zote kuna wengine watakuja na kufanya vizuri zaidi yake kama waliokuwepo mwanzoni ambao kwasasa baadhi wamechuja hivyo yeye anaitumia vizuri fursa aliyonayo sasa.

No comments:

Post a Comment