Tuesday, July 1, 2014

Mafanikio Ya Diamond Platnumz Yananinyima Usingizi: Linex

Linex
Mafanikio ya mwanamuziki Diamond Platnumz baada ya kuwa nominated katika tuzo za BET Awards, MTV Africa na AFRIMAA yanaonekana kuanza kuwazinduwa wasanii wenzake wengi na kuatamani wangekuwa Diamond. Mwanamuziki Linex ameamua kuweka wazi hilo kwa kusema kuwa mafanikio ya Diamond yanamnyima usingizi lakini sio kwa ubaya ili na yeye kutaka kufika alipo Diamond na hata kumpita.


 Kupitia mtandao mmoja wa kijamii Linex ameandika "kutoka moyoni this step ya huyu mwana inaninyima usingizi but haininyimi kwa ubaya ila inaninyima kwa uzuri na inanipa msukumo wa kupiga kazi na kuamini Mungu aliweka kitu ndani yangu kwa makusudi big s/o Diamond Platnumz ninachoamini mimi umefungua njia muziki wa Tanzania #wema kwa ubaya # we the voa"

Linex aliongeza kwa kuandika "Watu wanachukulia poa lakin @diamondplatnumz kafanya kitu kikubwa na hakijawah kutokea nchi hii so kila mtanzania anapaswa kua proud na mwana alichokifanya#uzalendo'

Imefikia wakati sasa kwa wasanii wa Tanzania kuacha majungu na kuungana katika kufanya kazi za kimataifa na kupata hamasa ya mafanikio na inspiration kupitia kwa Diamond kama alivyosema Linex. Si lazima Diamond ila kikubwa kufanya kazi za kimataifa.

Like our Facebook page Swahili World Planet for more updates about Tanzanian movie stars' latest gossips, news, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news

No comments:

Post a Comment