Pages

Thursday, June 26, 2014

VAD Film Productions Wapanga Kufungua Matawi Ya Kuuza Kazi Zao Nchi Mbalimbali.

Wasanii wa kundi la VAD wakiwa katika kikao cha pamoja
Kundi la VAD Film Productions toka Denmark ambalo linamilikiwa na waafrika waishio nchini humo kuanzia mwaka kesho wana mpango wa kufungua vituo vya kazi zao katika nchi mbalimbali na kufanya kazi na watu tofauti ambao watakuwa na uhitaji wa kazi zao. Vituo hivyo vitakuwa ni kwa ajili ya kuuza kazi zao za filamu kwa watu wanaozipenda ambao kwasasa inakuwa vigumu kuzipata kutokana na soko lao kutofika nchi nyingi kwa sasa.
Hivi juzi VAD walifanya mkutano wa pamoja kwa ajili ya mikakati yao hiyo ya kukuza soko la kazi zao ambapo pia watatoa vitambulisho kwa kila kituo cha kazi zao kwa wale wataopenda kufanya kazi nao. Kwasasa wanakamilisha michakato yote ikiwemo mawasiliano ya namna ya kuwapata kwa atakayehitaji kufanya kazi nao. Utazipata habari hizo hapa hapa SWP mchakato utakapo kamilika

Bango lenye baadhi ya picha za wasanii wa VAD karibu na ofisi zao
Vitambulisho vya VAD
Like our Facebook page Swahili World Planet for more updates about Tanzanian movie stars' latest gossips, news, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news

No comments:

Post a Comment