Pages

Sunday, June 15, 2014

Semina Ya Waandishi Wa Miswada Ya Filamu(script writing) Kufanyika Tarehe 19-21 June.

Bishop Hiluka mwezeshaji
SEMINA kubwa imeandaliwa kwa waandishi wa miswada ya filamu (Script writing) kwa wadau wote wa tasnia ya filamu Swahiliwood, semina hiyo itaendeshwa na mkufunzi wa kimataifa Bishop J. Hiluka, ili uweze kushiriki utatakiwa kujiandikisha na kulipa gharama 18,000 ya chakula kwa siku tatu.
“Chama cha waandishi wa script kimeandaa semina kwa wadau wa filamu wote wanachama na wale ambao si wanachama, lengo likiwa ni kujielimisha zaidi, hivyo tunatoa wito washiriki wajitokeze kwa wingi,”anasema Kingalu mwenyekiti wa muda wa chama hicho.

USIKOSE SEMINA HIYO MUHIMU ISIYO NA GHARAMA ZAIDI YA CHAKULA TU, Kwa wale wanaopenda kushiriki katika mafunzo hayo yanayoanza tarehe 19, 20 na 21 mwezi huu. Yanafanyika kwa mpango wa TAFF kuwawezesha wasanii kupata elimu kwa njia rahisi, kwa wale wanaotaka kushiriki wapige simu namba : 0713 626 252, 0783 359 999.

credit: Filamucentral

Like our Facebook page Swahili World Planet for more updates about Tanzanian movie stars' latest gossips, news, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.

No comments:

Post a Comment