Pages

Wednesday, June 18, 2014

Nasir Mohamed Ashinda Best Scriptwriter Na Kutwaa $2,000 Zanzibar International Film Festival 2014.

Nasir Mohamed akiwa na furaha
Nasir Mohamed ambaye ni muongozaji na producer wa filamu nchini kwa muda sasa ameshinda tuzo ya uandishi bora wa Script katika Zanzibar International Film Festival inayoendelea sasa huko Zanzibar. Kwa ushindi huo Nasir amepata zawadi ya dola $2,000 za kimarekani takribani Tsh. 3,363,000, katika shindano hilo kulikuwa na majaji maalum walikuwa wakitoa maksi na kukosoa washindani.

Miongoni mwa waliokuwa wakichuna na Nasir ambao waliingia final hiyo ya shindano ni pamoja na Zagamba Junior, Ali Yakuti, Arnold Mwalugelo, Emmanuel Mzava, Erick Makoti, Fredrick Shirima, Gabriel Kami, Halid Tolbert, Hassan Mambo, Irene Sanga, Martin Mahimbo, Nyachiro Kasese, Surchyang Raphael, Na Zakaria Riwa. Hongera sana kwa Nasir Mohamed kwa ushindi huo na ni matumaini yetu watengeneza filamu nchini wataona uwezo wako wa kikazi na kukutumia kwa kuacha mazoea ya kubebena hata kama kazi ni mbovu.

Hongera pia kwa washindani wote waliongia final katika mchakato huo tunaamini kazi zao pia ni nzuri ila siku zote mshindi huwa mmoja.
washiriki wakiwa katika picha ya pamoja
Like our Facebook page Swahili World Planet for more updates about Tanzanian movie stars' latest gossips, news, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news

No comments:

Post a Comment