Pages

Saturday, June 21, 2014

Msambazaji Kuinunua Filamu Mpya Ya Wema Sepetu Kwa Mil.90 Bila Kununua Haki Zote !

Wema Sepetu
Habari mpya zilizoifikia Swahiliworldplanet ni kuwa kuna uwezekano mkubwa Wema Sepetu akalipwa shilingi mil.90 za kitanzania kwa kuiuza filamu yake mpya kwa msambazaji mmoja anayekuja juu kwa kasi pasipo kuuza haki zote za filamu yake hiyo mpya ikidaiwa msambazaji huyo amekuja na kanuni mpya ya kutonunua haki za wasanii kutokana na malalamiko ya muda mrefu ya wasanii kwa wasambazaji wengine.
Kwa mujibu wa chanzo kimoja kilicho karibu na Wema kimesema kuwa filamu hiyo yupo pia Aunty Ezekiel na Hemedy. "kuna uwezekano Wema akalipwa mil.90 kuuza movie yake mpya alocheza na Aunty na Hemedy na ......(akimtaja msambazaji) lakini hawajamalizana bado unajua wasambazaji wengine wamemfata madam pia but yeye hayupo tayari kuuza kwa bei ndogo kama wengine, si unajua sokoni anauza fresh" kilisema chanzo hicho kwa masharti ya kutotajwa jina

Hata hivyo Wema hakupatikana kuzungumzia suala hilo ingawa takribani mwezi mmoja uliopita mmoja wa maproducer wa filamu nchini alisema pia kuwa amesikia kuwa Wema atalipwa pesa nzuri kwa filamu yake mpya anayo-shoot akiwa na Aunty Ezekiel na Hemedy ingawa habari hiyo haikuandikwa. SWP ilipojaribu kumuuliza mmoja wa wafanyakazi wa kampuni hiyo alisema hajui hilo na pia yeye siyo mzungumzaji wa kampuni kwa hiyo hana lolote la kusema kama ni kweli au sio kweli.
Wema
Like our Facebook page Swahili World Planet for more updates about Tanzanian movie stars' latest gossips, news, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news

No comments:

Post a Comment