Thursday, May 1, 2014

Kajala: Naogopa Hata Kushika Simu Yangu, Ugomvi Wetu Na Wema Sepetu Umekuzwa Na Watu Na Media.

Wema na Kajala
Kajala Masanja ambaye ni star wa filamu nchini amesema kuwa imefikia hatua anaogopa kushika simu yake kutokana na ugomvi wake na Wema Sepetu ambao amedai kuwa umekuzwa na watu na media kiasi cha kutokea kweli ugomvi baina yao lakini wao walitofautiana kwa kitu kidogo tu na cha kawaida  sio kama inavyodaiwa kuwa alimchukulia Wema mwanaume(Clement yule kigogo wa ikulu). Akizungumza katika kipindi cha TakeOne kupitia Clouds Tv Kajala alisema kuwa anaumizwa sana na hali hiyo na alishamwambia Wema wamalize tofauti zao lakini ikashindikana.


Kajala alipoulizwa kuhusu madai kuwa alianza kumdharau Wema baada ya kuanza kuyumba katika suala la pesa Kajala alipangua madai hayo kwa kusema kuwa walikuwa marafiki muda mrefu hata kabla Wema hajawa na pesa hivyo asingeweza kufanya kitendo hicho " alikuwa rafiki yangu kabla hana kitu, kwa hiyo madai kwamba nilianzisha urafiki na Wema kwasababu alikuwa na hela lakini sasa hivi hana hela tena mimi sio rafiki yangu tena sio kweli" alisema star huyo wa filamu za Devil Kingdom, Kigodoro na Kijiji Cha Tambua Haki.

Kajala aliongeza kwa kusema kuwa kutofautiana kwao kumemuathiri "inaniathiri sana kwasababu ni mtu ambaye nimemzoea, mtu ambaye tumefanya vitu vingi kwahiyo sometimes nikikaa nam-miss"

credit: Bongo5

 kusema kuwa kutofautiana kwao kumemuathiri "inaniathiri sana kwasababu ni mtu ambaye ni

No comments:

Post a Comment