Tuesday, May 20, 2014

JB Akatisha Ziara Yake Ya Uturuki Kuja Kumzika Adam Kuambiana.

Star mkubwa wa filamu nchini Jacob Stephen(JB) ambaye hivi majuzi walienda nchini Uturuki kwa ajili ya ziara ya kikazi kwa wiki mbili amekatisha ziara yake hiyo na kurudi nchini kuja kumzika msanii mwenzake Adam Kuambiana aliyefariki juzi. JB tayari alishafanya kazi kadhaa na Kuambiana kwani hata filamu yake mpya iliyotoka wiki kadhaa nyuma inayoitwa Hukumu Ya Ndoa Yangu imeongozwa na Kuambiana. Kupitia mtandao mmoja wa kijamii jana JB aliandika "Tumefanikiwa kupata nafasi moja tu ya kurudi Dar es salaam kwa ajili ya msiba .ahsanteni wenzangu kwa kukubali niwawakilishe, mbaki salama nawapenda.". Kuambiana anazikwa leo Jumanne .

Katika safari ya Uturuki ambayo imedhaminiwa na Princess Casino JB aliongozana na Ray, Irene Uwoya na King Majuto.

No comments:

Post a Comment