Wednesday, April 30, 2014

Wema Sepetu Na Najma Datan Walinifilisi Na Kuyumba Kiuchumi Baada Ya Kuwa Wapenzi: Mr.Blue

Mr.Blue

Mwanamuziki maarufu wa Bongofleva Mr. Blue amesema kuwa wasanii wa filamu nchini Wema Sepetu na Najma Datan ambaye pia ni mwanamuziki wa Bongofleva akiwa pia ameishi UK kwa muda mrefu walimfilisi wakati alipokuwa nao kimapenzi kwa nyakati tofauti kutokana na kuendekeza matumizi ya pesa nyingi na starehe
Akizungumza na Globalpublishers Mr. Blue ambaye aliyeanza kupata umaarufu akiwa bado kijana mdogo, alisema alilazimika kutumia fedha nyingi akiwa nao, kwani vinginevyo wangemuona hana pesa, kitu ambacho hakuwa tayari kuona kinatokea.
Mr.Blue na Najma Datan
"Mademu wengi walikuwa wanapenda sana starehe, kila day (siku) wanataka twende kiwanja, ndiyo maana kama unakumbuka niliyumba kimuziki"
"Wanawake wengi niliotoka nao hawajulikani, ila kuna Wema na Najma, ilikuwa ukizama nao dukani lazima ufanye shopping (manunuzi) ya nguvu, kuanzia laki saba, nane na kuendelea ili wakuone unazo na mademu wengi wakisikia tu umepiga shoo, sms hazikauki kuomba uwatumie mawe (pesa),” alisema.
Kuhusu maisha yake ya sasa, Mr. Blue alisema yamebadilika sana, kwani hivi sasa ameoa mwanamke mwenye asili ya Kiarabu na amejaliwa kupata mtoto mmoja, hivyo ni baba wa familia ambaye pia anakaribia kumaliza mjengo wake siku si nyingi.
Hata hivyo alisema mkewe siyo maarufu, ana malengo na upendo kwani amekuwa akimuaga kila safari anayofanya na kwamba hata yeye anaporejea nyumbani, hupokelewa vizuri.



Mr. Blue ni mmoja kati ya wasanii wa muda mrefu ambao bado wanafanya muziki na wenye mashabiki wengi ndani na nje ya Tanzania.

                                                                          Wema
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Filamu kali ya SIO SAWA inaingia sokoni Ijumaa hii April 2014 hakikisha unanunua nakala yako halisi.
Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news, life styles news and more

No comments:

Post a Comment