Monday, April 28, 2014

Odama Afurahi Na Kufunguka Baada Ya Filamu Ya Jicho Langu Kufanya Vizuri Sokoni.

Odama
Habari zisizo na shaka ni kuwa filamu mpya ya Odama Jennfer Kyaka inayoitwa JICHO LANGU ambayo imetoka wiki kadhaa zilizopita imefanya vizuri sokoni kwa mauzo kuliko filamu yoyote ile ambayo alitengeneza star huyo. Chanzo kimoja kilicho karibu na muigizaji huyo mwenye jina kubwa kikizungumza na Swahiliworldplanet kilisema "Jicho Langu ya Odama imefanya vizuri sana juzi alienda Steps kuangalia takwimu za mauzo na ndiyo filamu yake iliyouza sana katika zote alizawahi kutengeneza". Odama mwenyewe alipoulizwa na SWP kuhusu mwenendo wa filamu hiyo sokoni alisema "namshukuru Mungu filamu imefanya vizuri sokoni"

 Ukiachilia mbali story nzuri na waigizaji kucheza vizuri chanzo hicho kiliongeza kwa kusema kuwa promo iliyopigwa kwa ajili ya kuitangaza filamu hiyo ikiwemo hapa Swahiliworldplanet ilisaidia kufanya vizuri huku Odama mwenyewe akiishukuru Swahiliworldplanet kwa support ya kuitangaza filamu hiyo.

Filamu hiyo licha ya Odama mastaa wengine waliocheza ni Salim Ahmed "Gabo zigamba", Thadeo Alexander na Grace Mapunda.

Kama bado hujaitazama filamu hii basi wahi sasa kununua copy yako halisi kabla haijaisha madukani.

xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Filamu kali ya SIO SAWA inaingia sokoni Ijumaa hii April 2014 hakikisha unanunua nakala yako halisi.
Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news, life styles news and 

No comments:

Post a Comment