Wednesday, April 30, 2014

Batuli Aitikisa Ndoa Ya Mtunisy,

Batuli
Star wa filamu Swahiliwood Yobnesh Yusuph "Batuli" anadaiwa kuitikisa ndoa ya star mwenzake wa filamu Nice Mohamed "Mtunisy" ambaye waliwahi kuwa wapenzi kipindi cha nyuma kwa miaka kadhaa kabla ya kumwagana. Chanzo kimoja kikizungumza na Globalpublishers kwa sharti la kutotajwa jina lake gazetini kilifunguka kuwa issue ya wawili hao kuwa wapenzi siyo siri, kwani mara kadhaa wamekuwa wakijiachia sehemu mbalimbali, huku mke wa Mtunis akinyetishiwa, jambo lililosababisha migongano ndani ya ndoa hiyo.

"Mmechelewa kweli kujua! Leo ndiyo mnauliza kuhusu Mtunis na Batuli? Hao ni wapenzi na penzi lao limenoga kwelikweli sasa hivi. Imefikia hatua Mtunis na mkewe hawana maelewano mazuri. Nyumba ni kama inayumbishwa na Batuli lakini Mtunis hataki kumwacha Batuli,” kilipasha chanzo hicho.
Mtunisy
Kwa upande wa Mtunisy ambaye filamu yake mpya ya Jike Dume inaingia sokoni tarehe 1 mwezi May alipotafutwa na mtandao huo na kuulizwa alikana madai hayo kwa kusema "Kwanza nani amekuambia kuwa mimi natoka na Batuli? Yule ana mtu wake na mimi nina ndoa yangu. Sikia kaka, katika kipindi ambacho ndoa yangu ina amani ni hiki, sitaki kabisa haya mambo. Mtakuja kusababisha Batuli agombane na mumewe kisa mimi"
Batuli alipotafutwa kwa njia ya simu, alikuwa msikivu muda wote alipoelezwa kuhusu madai hayo, mwishoni akajibu kwa mtindo wa kuuliza: “Kwanza nikuulize, Mtunis ni Muislam au Mkristo?”
Mwandishi alipomjibu kuwa ni Muislam, akaendelea: “Sasa kipi cha ajabu hapo? Kwa imani yake ya Kiislam, ana ruhusa ya kuoa wake hadi wanne. Halafu kuna wakati nilishaishi naye miaka si chini ya minne, kwa hiyo sioni ajabu hapo. Hata kama ikitokea tena hakuna tatizo" 

Batuli aliyejaaliwa mvuto wa haja alimalizia kwa kusema "Achana na watu bwana, acha tu watu waongee. Lakini ninachosema hakuna cha ajabu hapo. Maisha yanaruhusu, yaani kisheria hata Mungu anaruhusu - siyo ajabu. Siwezi kuzungumza zaidi maana nimesafiri nipo kwenye harusi, dada yangu anaolewa"
                                                           Batuli
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Filamu kali ya SIO SAWA inaingia sokoni Ijumaa hii April 2014 hakikisha unanunua nakala yako halisi.
Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news, life styles news and 

No comments:

Post a Comment