Watanzania Hawathamini Mastaa Wao Nitaolewa Na Mwanaume Wa Nje. Jackline Wolper
Star mkubwa wa filamu nchini Jacqueline Wolper
ameibuka na kudai kuwa, atafanya kila njia ili aolewe na mwanaume wa nje
ya nchi na siyo Wabongo ambao hawathamini mastaa.
Akizungumza
na Uwazi, Wolper alisema, amefikia uamuzi huo kwa sababu ana uchungu
moyoni unaotokana na dhana waliyonayo wanaume wa Kitanzania juu yao,
wakiamini kuwa ni wahuni tu hivyo kuwashusha thamani.
“Unajua
Mtanzania anamchukulia staa kama chombo cha starehe tu na hawezi kumuoa
kamwe na hata akimuoa basi hatamthamini kama wanavyothaminiwa wasanii
wa huko nje.
“Kule
bwana (hajataja nchi) mtu akimuoa staa, anampa kipaumbele. Anaweza hata
kutumia fedha kuhakikisha anakuwa na staa na maisha ya mke wake
yanakuwa yenye amani lakini hapa kwetu tunadharaulika sana ndiyo maana
nimefikia uamuzi huu,” alisema Wolper na kuongeza:
“Unajua
Watanzania wanaamini staa kuandikwa magazetini ni uhuni lakini
wanasahau kuwa maisha yake na magazeti ni kitu cha kawaida kwa sababu ya
kujulikana. Mimi sina haja ya kueleza sana lakini naapa kabisa, mimi
siwezi kuolewa na Mbongo.”
Follow us on twitter Swahili World Planet and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP
for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities,
features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and
Nollywood news, life styles news and more
No comments:
Post a Comment