Sunday, March 23, 2014

Ray C Katika Mikakati Mizito Ya Kumpindua Wema Sepetu Katika Penzi La Diamond.

Ray C
Ray C ambaye anajipanga kurudi kwa kasi katika muziki wa Bongofleva anadaiwa kulimezea mate penzi la Diamond Platinumz huku akihaha usiku na mchana kumpata kwa kumpindua Wema Sepetu ambaye kwasasa ndiye anayefaidi kwa Diamond. Chanzo kimoja kilicho karibu na star huyo kikizungumza na Swahilitz kilisema kuwa kwasasa jina la Diamond halikauki mdomoni mwa Ray C ambaye alitamba sana katika muziki miaka michache nyuma "kwasasa Ray C haambiwi kitu kwa Diamond, ana haha kila wakati kumweka mikononi mwake, hana furaha kabisa hadi lengo lake litakapotimia, na muda si mrefu mtaandika juu ya hao"


Inadaiwa Ray C amekuwa akipanga miadi ya kuonana na Diamond mara kadhaa bila mafanikio lakini furaha yake itatimia akilinasa penzi la Diamond ambalo linawindwa na wasichana wengi. Ray C alipotafutwa na mtandao huo kutolea ufafanuzi madai hayo simu yake ilidaiwa kuwa busy muda wote. Kwa upande mwingine Diamond alipotafutwa na kupatikana alisema "kaka mimi sina taarifa kabisa na habari hizo, kwangu Ray C namchukulia kama dada yangu" Diamond alipododoswa zaidi kuwa je kama Ray C akijitokeza na kumtamkia wazi kuwa ameoza juu ya penzi lake atachukua uamuzi gani, Diamond alijibu kwa ufupi kwa kusema "No Comment (sina cha kujibu)" halafu akakata simu haraka






Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news, life styles news and more

No comments:

Post a Comment