Monday, February 3, 2014

JB, UWOYA, JOHARI, SLIM, MBOTO, BABA HAJI, AMANDA,WASTARA WAJIUNGA CCM, JOYCE KIRIA AWAPONDA.

Wasanii kadhaa wa filamu nchini wamehudhuria sherehe za maadhimisho ya miaka 37 ya CCM na pia kudaiwa kuwa wanachama na kuchukua kadi kwa ambao hawakuwa wanachama.  Wasanii hao ni kama Jacob Stephen(JB), Irene Uwoya, Johari, Wastara Juma, Slim Omar, Baba Haji, Single Mtambalike(Richie), Amanda Poshy na wengineo kama wanavyoonekana pichani hapo juu. Hata hivyo baadhi ya wadau wa filamu wamedai kuwa wasanii hao wanao uhuru wa kuchagua chama chochote lakini inaonekana wamekurupuka kwasababu serikali ya chama hicho hicho ndiyo ambayo imeziba masikio kuwasaidia wasanii miaka nenda rudi kwa kutokuweka miundo mbinu mizuri kwa ajili ya kunufaika na kazi zao.



Inadaiwa wasanii hao wameanza kuonekana ni muhimu katika kipindi hiki cha kuelekea katika uchaguzi mkuu wa 2015 ambapo kundi la wasanii huwa na ushawishi katika jamii hivyo chama hicho kuwatumia ili kupata kura zaidi.

Ukiachilia mbali waliolalamikia wasanii hao kuwa hawajitambui kwa maana kuwa watatumiwa katika kipindi hiki cha shamra shamra za kuelekea uchaguzi mkuu wa 2015 na baada ya hapo kuonekana hawana thamani tena lakini wengine wameona ni sawa tu walivyoamua kwani ni haki yao kikatiba kuchagua chama chochote kile. Inadaiwa kuwa wasanii wengi waliojiunga CHADEMA ambacho ndiyo chama pinzani kwa CCM ni wanaharakati tangu hawakujiunga na wana uchu wa kumkomboa msanii ili afaidike na kazi zake, wasanii waliojiunga CHADEMA ni kama vile Lady Jaydee, Afande Sele, Professor J, Sugu ambaye kwasasa ni mbunge wa mbeya mjini na wengineo.

Naye Joyce Kiria ambaye anadaiwa kuwa mwanzilishi wa jina Bongo movies amewachana wasanii hao kwa kuandika  ...............

Kila mtu anao uhuru wa kuchagua chama atakacho hasa akiona kama kinamfaa, Je wewe una maoni gani kwa wasanii hawa ambao kila siku wanalia kazi zao kuibiwa, kutonufaika na kazi zao lakini serikali iliyopo madarakani haiwasikilizi?, Unadhani kujiunga kwao CCM itakuwa suluhisho la matatizo yao?




Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news, life styles news and more

No comments:

Post a Comment