Pages

Sunday, January 19, 2014

RAYUU AFUNGUKA MADAI YA KUTOKA KIMAPENZI NA CYRIL KAMIKAZE.

Rayuu
Rayuu ambaye ni muigizaji wa filamu Swahiliwood amekanusha madai ya kuwa anatoka kimapenzi na mwanamuziki wa Bongofleva Cyril Kamikaze. Wiki iliyopita Swahiliworldplanet ilitonywa na chanzo kimoja kuwa Rayuu na Kamikaze ni wapenzi na hivi karibuni walikuwa wana-shoot filamu mpya na kuamua kujirusha kabisa kunako sita kwa sita. " Rayuu mpenzi wake ni Cyril Kamikaze sasa hivi, niliwaona location juzijuzi tu na walikuwa kimahaba sana, walivunja amri ya sita" kilisema chanzo hicho ambacho kimetokea pamoja na Rayuu kwenye video moja ya mwanamuziki wa Bongofleva



Hata hivyo Rayuu alipotafutwa na kuulizwa kama ni kweli kwasasa anajibana kwa Cyril Kamikaze alipangua madai hayo kwa kusema " hapana sisi ni marafiki wa kawaida tu ila tulikuwa tunashut movie mpya ndiyo maana watu wameshazusha kuwa sisi ni wapenzi, Cyril ni rafiki yangu tunawasiliana kawaida tu"

                                                                 Cyril Kamikaze
Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news, life styles news and more

No comments:

Post a Comment