Pages

Wednesday, January 22, 2014

PHOTOS: DIAMOND ATIMIZA AHADI YAKE YA KUWASOMESHA WATOTO WALIOSHINDA KUCHEZA NGOLOLO.

Licha ya kwamba mwanamuziki superstar wa Tanzania Diamond Platinumz hakufanikiwa kusoma kwa kiwango cha juu lakini bado anathamini na kuona umuhimu wa elimu kwa mtoto na mtu yeyote yule katika ulimwengu wa sasa ulioshikiliwa na utandawazi ambapo elimu huwa moja ya silaha muhimu sana. Kupitia mtandao wake jana Diamond aliweka picha za kutimiza ahadi yake ya kuwasomesha watoto walioshinda katika shindano la kucheza Ngololo ambalo lilifanyika mwishoni mwa mwaka jana katika show yake.



Watoto hao watasomeshwa katika shule ya East Africa International School iliyopo Mikocheni jijini Dar es salaam na jana hiyo hiyo Diamond alitinga shuleni hapo kuwaandikisha watoto hao tayari kuanza masomo. Diamond ambaye umaarufu wake upo mpaka nje ya Tanzania aliandika ....................

Angalia picha hapo chini Diamond akitimiza ahadi yake ya kuwasomesha watoto hao...................

Diamond akisalimiana na mkuu wa shule hiyo....

Diamond akiwa ofisini kwa mkuu wa shule hiyo tayari kuwaandikisha watoto hao kuanza shule

Watoto waliopata bahati ya kusomeshwa na Diamond baada ya kushinda kucheza Ngololo ndiyo hawa

Diamond  akiwa na wazazi wa watoto hao ofisini kwa mwalimu mkuu


Diamond akiwa na wanafunzi wanaonekana kuwa mashabiki wake
Hongera sana Diamond kwa kuwasomesha watoto hao.................


all images by Wasafi(This is Diamond)



Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news, life styles news and more

No comments:

Post a Comment