Monday, January 13, 2014

KUTANA NA MALIK NYUMBA MMOJA WA CAMERAMEN / EDITORS WAZURI WA FILAMU NCHINI.

Malik Nyumba
Malik Nyumba ni mmoja wa cameraman na editors wenye uwezo mzuri katika tasnia ya filamu nchini ambapo amefanya kazi na baadhi ya wasanii wa filamu kadhaa nchini kama vile Jacob Stephen(JB), Elizabeth Micahel(Lulu), Odama Jenifer Kyaka na wengineo. Swahiliworldplanet ilipata nafasi ya kuchonga machache na Malik kuhusiana na kazi zake hizo za filamu na kwa kueleza...



" Nilianza kufanya kazi kwenye kampuni ya JB Jerusalem, movie ya kwanza kuifanya pale ni Dereva Taxi ikaja Vita Baridi pia nimefanya movie ya Lulu Foolish Age nikatoka pale kutokana na malipo madogo nikahamia kwenye kampuni ya Odama J-Film 4 Life mpaka sasa nipo hapo kama editor na cameraman movie ya kwanza kuifanya kwa Odama ni Family War ikaja Figo, Whitch doctor, Jicho na Inside ambazo hazijatoka pia nimefanya kazi na Mr. Chuzi movies kama 3 ila naikumbuka 1 inaitwa Dirty Game" alisema Malik. 

Kama wewe ukipenda kufanya kazi na cameraman/editor huyu basi wasiliana nae hapa Malik Nyumba

Baadhi ya kazi alizofanya ni hizi...........


Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news, life styles news and more

No comments:

Post a Comment