Friday, January 17, 2014

JACKLINE WOLPER AMUWEKA WAZI MPENZI WAKE MPYA.


Star wa filamu nchini, Jackline Wolper ameamua kumuweka bayana mchumba wake wa sasa anayejulikana kwa jina la G. Modo baada ya kukaa kimya muda mrefu tangu alipoachana na Abdallah Mtoro ‘Dallas’.
 
Jacqueline Wolper akiwa na mchumba wake wa sasa G. Modo.

Akizungumza na Globalpublishers Wolper alisema alikuwa kimya kwa muda mrefu kwa ajili ya kutafakari kwanza maana asingeweza kukurupuka wakati bado hawajachunguzana tabia vizuri na mpenzi wake huyo.

“Kiukweli nafurahia sana uhusiano wangu wa sasa na siwezi kusema moja kwa moja kuwa ndiye mume wangu kwa vile najua kila kitu kinaongozwa na Mungu, ninachokiomba ni ndoto yangu ikamilike tu kwani nahisi niliyempata ni sahihi kwangu,” alisema Wolper.

Wolper aliongeza kuwa kama siku Mungu atajalia kwa mpenzi wake huyu kitakachofuatia ni kwenda moja kwa moja  kwa wazazi wa pande zote mbili ili kupata baraka na ndiyo kitu ambacho anakiomba kila kukicha.



Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news, life styles news and more

No comments:

Post a Comment