PHOTOS: EMMANUEL MSUYA AIBUKA MSHINDI WA BONGO STAR SEARCH 2013 NA KUJINYAKULIA MILLIONI 50.
Kinyanganyiro
cha kumtafuta Super Star wa Bongo kupitia Epiq Bongo Star Search 2013
kimekamilika alfajiri hii kwenye ukumbi wa Escape 1.
Mashindano
haya ambayo kidogo yalichelewa kuanza yalipambwa na wasanii mbalimbali
wakiwemo Barnaba,Makomando,Young Killer,water chilambo,Shaa,Kimbunga na
Snura.
Katika mashindano haya ambayo yalikua na jumla ya washiriki watano
ambao ni Amina Chibaba,Elizabeth Mwakijambile,Emmanuel Msuya,Maina
Thadei na Melisa John,ambao walipita kwa round tatu kisha majaji
kuwapunguza watatu na kisha kubakia Emanuel Msuya na Elizabeth
Mwakijambile katika Round ya 4 na ya mwisho.
![DSC_0098](https://lh3.googleusercontent.com/blogger_img_proxy/AEn0k_t_T4e0FSecm5zKno2WohlQrIU60aoYJMBqxUHzFCxeuwlyGecT03UCwCrGUxV9XFog5a-TILNWCePkGG7uj7FUmpMTbcNCbVfBddN9cvzzx1gb-PDoCSb6APFweM0HAjI=s0-d)
Katika
round ya mwisho,Emmanuel Msuya ameibuka kidedea na kuwa Mshindi wa Epiq
Bongo Star Search 2013,akiwa ni mshiriki anaetokea Jijini Mwanza na
kumpokea taji water chilambo ambae alikua mshindi wa mwaka jana.
Zawadi kwa mshindi wa mwaka huu ni Milion hamsini[50]ambayo kakabidhiwa jukwaani.
images by
Millardayo
Follow us on twitter Swahili World Planet and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP
for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities,
features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and
Nollywood news.
No comments:
Post a Comment