"Vyombo vya habari vya Nigeria vilituweka kwenye ramani, wanamuziki wenu wanafanya kile kile sisi tunachokifanya. mnawaona watu hawa hapa(Lady Jaydee, Ben Pol na Professor J) mnaweza kuwafanya wawe wakubwa kuliko P-Squere. Ukweli ni kwamba tuna-promot muziki wa Afrika, waafrika huu ni muda wetu. wamarekani nasema wanaogopa sasa hivi, ningependa kuona mnaweka jitihada zaidi kwa wanamuziki wenu hapa. nataka kuwaona wanakuja Nigeria na kuongoza concert, hakuna mtu anayeweza kufanya hivyo vizuri isipokuwa nyinyi(vyombo vya habari)" alisema Peter Okoye
"wanaigeria walifanya hivyo kwetu, nyinyi mnaweza kufanya hivyo kwa Jaydee, Professor J na wengine" alisisitiza Paul Okoye
P-Squere wamesema hayo huku baadhi ya vyombo vya habari kuanzia Radio, Tv, magazeti na mitandao ikiwa na kasumba ya kuwapuuza wasanii wa Tanzania na kuwabeba zaidi wale wa nje kitu ambacho sio sahihi hata kidogo. Kama walivyosema P-Squere kuwa vyombo vyao vya habari vimeonyesha uzalendo ndiyo maana hata huku leo tunawajua, wasanii wa marekani leo tunawajua na kuwaona wapo juu lakini hiyo imetokana na mchango wa vyombo vyao vya habari. Inasikitisha mpaka sasa kuna baadhi ya magazeti nchini na vituo vya Tv vinaandika habari za waigizaji wa Nigeria na kuonyesha filamu zao kwa kiasi kikubwa na kutowapa nafasi wale wa Tanzania kwa uzito mkubwa, shame on you..!!!!. baadhi ya vituo vya radio vinavyojiita vya kijanja vinatoa kipaumbele kwa wanamuziki wa nje na sio wa Tanzania. na sasa P-Squere wameamua kuwazodoa nje nje..!!. Siku zote mjenga nchi ni mwananchi mwenyewe. Tumeona jinsi gani wasanii wa Tanzania wanavyopokelewa kishujaa nchi jirani kuliko hata badhi ya wasanii wa nje hii inaonyesha wanakubalika pamoja na kazi zao.
Huu unatakiwa uwe muda wa mabadiliko kwa vituo vya radio, Tv, magazeti na mitandao ya Tanzania kutoa sapoti zaidi kwa wasanii wa nyumbani na sio wa nje kwani vipaji tunavyo na uwezo tunao hao wa nje hawataliletea faida yoyote taifa hili zaidi ya kufaidisha na kutangaza nchi zao.
P-Squere
No comments:
Post a Comment