Millen Happiness Magese (kulia) akikagua baadhi ya miradi yake manispaa ya Mtwara.
17/11/2013: Mwanamitindo wa kimataifa wa Tanzania,
Millen Happiness Magese amewataka watu binafsi na makampuni mbalimbali
kujitokeza kwa wingi katika kusaidia tasnia ya elimu hasa katika maeneo
yasiyopewa kipaumbele ili kuwaokoa watoto wa maeneo hayo kutotumbukia
katika vitendo visivyo vya kimaadili. Rai hiyo ameitoa wakati
alipotembelea miradi yake aliyoifadhili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa
na utengenezaji wa madawati.
Millen akizidi kukagua miradi hiyo leo.
Ujenzi wa madarsa unaendelea katika shule ya msingi Mjimwema iliyopo
manispaa ya Mtwara ambapo mradi wa kutengeneza madawati ulikabidhiwa kwa
vikundi mbalimbali vya wajasiriamali mkoani hapo kwa mpango maalum
kupitia ofisi ya mkuu wa Wilaya, Mheshimiwa Wilman Ndile. Jumla ya
madawati hamsini na tano (55) yenye thamani ya shilingi milioni tano
yalikuwa tayari yameshatengenezwa kama walivyoahidi wajasiriamali hao
wakati wakikabidhiwa kazi ya utengenezaji wa madawati hayo.
Millen akiwa pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi Mjimwema iliyopo manispaa ya Mtwara ambapo madarasa yanajengwa.
Madawati hayo yalikabidhiwa rasmi na Millen yalikabidhiwa kwa wanafunzi wa shule ya msingi Lilungu.
Kwa upande wa afisa elimu wa manispaa ya Mtwara Frola Aloys amewataka
wadau wa elimu kuonesha uzalendo wa hali ya juu kwa maeneo ya Kusini mwa
Tanzania huku mkuu wa shule ya msingi Lilungu Abdul Nangomwa akielezea
changamoto zinazoendelea kuikumba sekta ya elimu katika shule za msingi
wilayani Mtwara.
Millen akipozi na wanafunzi wa Shule ya Msingi Mjimwema nje ya darasa jipya linalojengwa na mrembo huyo.
Mbali na kukabidhi madawati Millen aligtembelea ujenzi unaoendelea
shule ya msingi Mjimwema na kutoa zawadi ya madaftari napenseli kwa
wanafunzi hao ambapo mpaka sasa shule in mikondo mitatu ambayo ni
kuanzia darasa la awali mpaka darasa la pili.
Ziara hiyo ya mrembo huyo aliyewahi kushika taji la Miss Tanzania
mwaka 2001, ni mwendelezo wa shughuli za kijamii anazozifanya nchini
Tanzania hasa katika kusaidia makundi yenye mahitaji maalumu na yale
yasiyopewa kipaumbele.
Mwanzoni mwa mwaka huu Millen Magese alitoa kiasi cha shilingi
milioni kumi na tano katika kusaidia huduma hiyo ya elimu katika
manispaa ya Mtwara.
credit:
Globalpublishers
No comments:
Post a Comment