Friday, November 1, 2013

LULU ATOA MSAADA WA PESA HOSPITALI YA OCEAN ROAD.

Actress Elizabeth Michael(Lulu) ametoa msaada wa pesa katika hospitali ya Ocean Road jijini Dar es salaam ili ziwasaidie wagonjwa wa kansa. Haijajulikana star huyo wa filamu ametoa kiasi gani na aliambatana na mama yake mzazi katika hospitali hiyo. Kupitia Instagram Lulu ameandika "naamini mimi sio mwema sana mpaka Mungu akaniwezesha kuona mwezi huu nikiwa mzima na mwenye afya. Kwa kutambua hilo nimeanza mwezi huu kwa kupita katika hospitali ya Ocean Road na kutoa mchango ili kuwasaidia wagonjwa wa cancer na tuwe na utaratibu wa kuwakumbuka wahitaji kwa chochote tulichonacho"

Mungu awe upande wako na akuzidishie zaidi Lulu

Lulu akiwa na mama yake mzazi akitoa msaada wa pesa katika hopspitali ya Ocean Road...
Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news

No comments:

Post a Comment