|
Wolper |
Jackline Wolper ambaye ni star wa filamu nchini amefunguka kuwa filamu yake
aliyoitoa kumuenzi marehemu Steven Kanumba iitwayo After Death
ilimlostisha kwa kuwa ilimpatia hasara kubwa. Akizungumza na
Globalpublishers Wolper ambaye anafanya vizuri kwasasa katika filamu alisema
"Nilitengeneza ile filamu kwa hela nyingi kidogo, kama milioni 35 au
40, nikafanya na uzinduzi pale Leaders Club uliogharimu kama milioni 13
hivi, lakini nilipokwenda kwa Wahindi wakanipa shilingi milioni 25,
yaani inakatisha sana tamaa"
Alisema
hasara aliyoipata na ambayo hata wasanii wenzake huipata inatokana na
uwepo wa wasambazaji wachache wa kazi za wasanii, kitu kinachowafanya
watu hao kujipangia bei bila kujali gharama ambazo wasanii wameingia katika
utengenezaji wake.
Cover la filamu hiyo
Follow us on twitter Swahili World Planet and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP
for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities,
features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and
Nollywood news.
No comments:
Post a Comment