MAANDALIZI
ya tamasha kubwa la filamu lijulikanalo kwa jina la Arusha African Film
Festival yanaendelea vizuri na kila kitu kinaenda kama kilivyopangwa,
tamasha hilo ambalo linategemegea kuonyesha zaidi ya filamu 70 kutoka
nchi 20, litambatana na utoaji wa semina ya utengenezaji wa filamu kwa
watengeneza filamu ambao watajisajili kwa ajili ya Semina hiyo ambayo ni
muhimu sana kwa watayarishaji na tasnia ya filamu kwa ujumla.
Akiongea
na FilamuCentral mmoja wa waratibu wa tamasha hilo Mary Birdi amesema kuwa ni
tamasha ambalo linaleta mabadiliko makubwa katika tasnia ya filamu
Swahiliwood, kwani watengeneza filamu kutoka sehemu mbalimbali watafika
na kubadilisha mawazo na watengezaji wa filamu wa Tanzania, ni muhimu
kila mdau akajipanga na kushiriki tamasha hili linalojenga.
“Ni
tamasha ambalo linajenga tasnia ya filamu nchini hasa pale watu wetu
wanavyopata workshop kwa ajili ya kazi wanazofanya, siku hizi teknorojia
inakwenda kwa kasi ni vema kupata shortcourse mara kwa mara, lakini ni
nafasi pia ya kutangaza Utalii wetu,”anasema Mary.
Tamasha
la AAFF litazinduliwa tarehe 29.November.2013 Mount Meru Hotel Jijini
Arusha wakati Semina itaanza rasmi tarehe 25. Novemba
November.
2013 sambamba na maonyesho ya filamu katika sehemu zifutazo Alliance
Francaise, Via Via, Mount Meru Hotel, Mango Tree, na New Arusha Hotel
tamasha hili kiingilio ni bure kabisa, Siku 7 USIKOSE KUSHUHUDIA FILAMU
KALI KUTOKA SEHEMU MBALIMBALI.
No comments:
Post a Comment