Tuesday, October 29, 2013

WEMA SEPETU AZIMIA MARA TATU KUFUATIA KIFO CHA BABA YAKE MZAZI.

Wema Sepetu amabye ni Miss Tanzania 2006 na pia muigizaji wa filamu Swahiliwood amezimia mara tatu ndani ya masaa saba juzi kufuatia kupata msiba wa baba yake mzazi balozi Abraham Isaac Sepetu ambaye aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali za juu katika serikali ya Tanzania. Wema alipatwa na hali hiyo baada ya kutoamini kuwa hatamuona tena baba yake mzazi ambaye alikuwa anampenda sana. Chanzo kimoja kikizungumza na GPL kilisema "Wema bado mdogo, katika maisha yake hakuwahi kupatwa na msiba mkubwa kama huu, kumpoteza baba yake kipenzi, ni jambo zito ndiyo maana mpaka sasa tunaongea ameshazimia mara tatu, yaani anazimia na kurejewa na fahamu."
Jumapili saa 7 mchana baada ya kurejewa na fahamu Wema alisema: "Nimeumia sana kwani huu ni msiba mkubwa kwangu, Baba yangu alikuwa nguzo imara katika maisha yangu, sikuwahi kufikiria kama ningepata msiba mkubwa kama huu, taarifa hizi wakati nazipokea nilijua kama utani lakini yote ni mipango ya Mungu, inaniuma sana"


Pole Wema mungu atakupa nguvu katika kipindi hiki kigumu...

Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news

No comments:

Post a Comment