Wednesday, October 2, 2013

MTUNISY AWAPIGA DONGO ACTRESSES WANAOJICHUBUA.

Muigizazji maarufu Swahiliwood Nice Mohamed(Mtunisy) amewapiga dongo baadhi ya waigizaji wa kike nchini waliongia kwenye mkumbo wa kujibadilisha ngozi zao kutoka kuwa weusi wa asili na kuwa na weupe wa kununua dukani maarufu kama kujichubua au wengine siku hizi huita 'kujipiga deki". Kupitia mtandao mmoja wa kijamii Mtunisy anayetamba sokoni na filamu nyingi aliandika "Morning wapendwa wangu, tukiwa tunasubiri kutatuliwa kwa kitendawili cha film yangu ya WJO'S BAD kitakachoteguliwa tarehe 16 nina wasiwasi mpaka kufikia mwaka 2020 sidhani kama kutakuwa na actress mwenye ngozi nyeusi kwani walio weusi washakuwa weupe na weupe ndio wamekuwa wachina"

Alichokisema Mtunisy kina point hasa kwa muigizaji anayejitambua hawezi kujichubua na sio muigizaji tu bali hata watu wa kawaida kujichubua si kuzuri kwa kuwa kuna madhara mengi kiafya ikiwemo kansa ya ngozi. kwa muigizaji inakuwa ngumu kumchezesha characters zenye asili ya kiafrika na kijijini kwani wengine wamejichubua mpaka ngozi kuwa na rangi zaidi ya tatu, nyeusi, nyekundu, njano, blue na kijani hujitokeza usoni kwa mtu aliyeathirika na matumizi ya mkorogo. Mara nyingi waigizaji wanaojichubua wakicheza scenes za vijijini hawavutii usoni kwani mashavu na uso huwa na viraka vyeusi au kahawia na kupoteza ule uasili wa kiafrika ,. Na ndiyo maana hata film makers wa wa Hollywood wanapotaka waigizaji kutoka afrika huwa wanataka wale wenye weusi wa asili au ngozi zao halisi kwa kuwa ndiyo waafrika halisi na sio wale wanaoukana uafrika kwa kujichubua. Vile vile kujichubua ni ishara ya kutokujiamini katika ngozi yako halisi kwa mujibu wa wataalaam wa saikolojia. BE PROUD AFRICAN!!!

                                                                   Mtunisy

Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news

No comments:

Post a Comment