Friday, September 20, 2013

TWIN SISTERS, FILAMU MPYA YA KISWAHILI KUTOKA NORWAY, YAWAKUTANISHA BASHIZI, SELEMBE TOKO, MAGGIE NA ISABELLE.

Twin Sisters ni filamu mpya ya kiswahili ambayo imetengenezwa nchini Norway na Patrick Bashizi ambaye ni mmiliki wa kampuni ya JDP Production. Bashizi anaishi nchini Norway lakini akiwa na asili ya Congo. Filamu hii imechezwa  na Bashizi, Selembe Toko anayeishi Denmark na Maggie Seluwa ambaye ni muimbaji/muigizaji na isabelle Petersen . Inatarajiwa kutoka hivi karibuni katika DVD na kuna uwezekano mkubwa ikasambazwa Tanzania pia kama si nchi zote za Afrika mashariki na kati .


Bashizi anasema kuwa wanatumia lugha ya kiswahili katika filamu licha ya kuwa ulaya ili kuzidi kuikuza lugha hii ambayo inawaunganisha watu wengi katika nchi mbalimbali hasa za kiafrika. Ukiachilia mbali Twin Sisters Bashiz ambaye ni muongozaji wa filamu pia ameshatengeneza filamu nyingine kama vile Jabuka, The Pain Of Love, Tears Of Money na Remember God ambayo imetengenezwa kwa lugha ya kiingereza. Angalia picha za uchukuaji wa filamu hiyo hapo chini.............



Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.

No comments:

Post a Comment